Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, marehemu Ayatollah Muhammad Ali Nasiri, mmoja wa walimu wa akhlaqi hawza, katika moja ya masomo yake ya maadili, alizungumzia mada ya "Husuda na Athari Zake za Kiroho", ambayo mada hiyo ni kama ifuatavyo:
"Husuda," kama moja ya maovu hatari zaidi ya kitabia, inashikilia nafasi mahsusi katika mafundisho ya Maimamu wa Ahlul Bayt (a.s).
Imam Sajjad (a.s), katika dua tukufu ya "Makarimul Akhlaq", kwa maneno ya kina, anamwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu kuutakasa moyo wa mwanadamu kutokana na vishawishi vya Shetani kama vile matamanio ya kupindukia, dhana mbaya, kusingizia watu na husuda.
Tofauti kati ya dhana ya husuda na wivu katika utamaduni wa Kiislamu
Qur’ani Tukufu imeelezea kwa uzito mkubwa tabia hii ya kulaumiwa, na katika aya mbalimbali ikiwemo aya ya 109 ya Surah Al-Baqarah na aya ya 54 ya Surah An-Nisaa imeeleza athari zake mbaya.
Jambo la kutafakari ni kwamba katika Surah Al-Falaq, mtu mwenye husuda amewekwa sambamba na viumbe hatari na wa kudhuru, kama wanyama wakali na wachawi, jambo linaloonesha kiwango cha hatari na tabia hii mbaya.
Katika kufafanua asili ya husuda, pamoja na tofauti yake na dhana ya ghibta.
Kwa mfano, pale mtu anapofurahi kwa kuona neema kwa mwingine na kutamani kupata neema kama hiyo, hisia hiyo huitwa "ghibta", ambayo ni jambo linalokubalika na kupendeza.
Lakini husuda hutokea pale mtu anapohisi maumivu kwa kuona neema kwa mwingine na kutamani ipotee kwake. Mtu wa aina hii, kwa hakika, anakuwa katika hali ya kumpinga Mwenyezi Mungu na kujaribu kupingana na ugawaji wa haki wa Mola.
Mwenye husuda ni mwenye kutoridhika na neema za Mwenyezi Mungu na ni mwenye kupinga mgawanyo Wake wa haki
Katika Hadithi Qudsi Nabii Musa (a.s), Mwenyezi Mungu anasema:
"Ewe mwana wa Imran! Usione wivu kwa watu kwa yale niliyowapa kutokana na fadhila Zangu."
Maneno haya ya Mwenyezi Mungu yanaeleza kwa uwazi kwamba mwenye husuda, kwa kweli, anapinga mgawanyo wa haki wa Mola na ni mwenye kutoridhika na ugavi Mwenyezi Mungu.
Katika historia ya binadamu, dhambi ya kwanza ilianza kutokana na husuda ya Ibilisi dhidi ya Nabii Adam (a.s), na mauaji ya kwanza yakatokana na husuda ya Qabil dhidi ya Habil.
Tabia hii ya kulaumiwa si tu kwamba huondoa utulivu wa mwenye husuda, bali humweka katika mateso ya kiroho na kimwili yasiyoisha.
Kisa cha ndugu zake Nabii Yusuf (a.s) ni mfano wa kuzingatiwa, husuda haimdhuru tu anayehusudiwa, bali huenda ikawa ni sababu ya kuinuliwa daraja lake mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Maoni yako